Kuna wakati watoto wa mjini walipiga hela kiulaini sana. mtu aliivizia nguzo ya umeme usiku pasipo na watu, akaibandika karatasi lililoandikwa “Mpigie Mganga wa Ndoto”.
Chini akaweka namba kwa maandishi makubwa na wino uliokolezwa zaidi. Watu wakaota, wakapiga simu naye akawajibu baada ya muamala wake kusoma. Ni rahisi sana, haina Brela wala TRA.