Trump Aahirisha Mashambulizi Iran Kwa Siku Tano, Atoa Nafasi Ya Mazungumzo – Video

Global Publishers
March 23, 2026
0 Comments

Rais wa Marekani, Donald Trump leo Machi 23, 2026 ametangaza kuahirisha mashambulizi yaliyokuwa yamepangwa kufanywa dhidi ya mitambo ya umeme na miundombinu ya nishati nchini Iran kwa kipindi cha siku tano.

Kupitia taarifa yake rasmi, Trump amesema uamuzi huo umefikiwa kufuatia mazungumzo yaliyodumu kwa siku mbili kati ya Marekani na Iran, ambayo ameyataja kuwa yalikuwa mazuri, yenye tija na yaliyotoa mwelekeo mpya wa kumaliza uhasama uliodumu kwa muda mrefu katika ukanda wa Mashariki ya Kati.

Ameeleza kuwa mazungumzo hayo yanatarajiwa kuendelea katika siku zijazo, huku akisisitiza kuwa hatua ya kuahirisha mashambulizi inalenga kutoa nafasi kwa diplomasia kufanikisha suluhisho la kudumu.

Trump amebainisha kuwa hatua inayofuata itategemea mafanikio ya mazungumzo hayo, akionyesha matumaini kuwa pande zote mbili zinaweza kufikia makubaliano yatakayomaliza kabisa mvutano uliopo.

Hata hivyo, amewashukuru wadau wote wanaofuatilia mchakato huo na kusisitiza umuhimu wa kuendeleza juhudi za amani ili kuhakikisha utulivu katika eneo hilo.