Zaidi ya madaktari bingwa 30 kutoka China na Tanzania wanatarajiwa kuweka historia mpya ya huduma za afya jijini Dar es Salaam, kwa kuanzisha kambi maalum ya matibabu ya bure itakayodumu kwa siku mbili mfululizo, Machi 28 na 29, mwaka huu.
Kambi hiyo itafanyika katika viwanja vya East Africa Commercial Logistics Centre (EACLC), ikiwa ni jitihada za pamoja za wadau wa afya kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora bila gharama yoyote.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando, amewataka wakazi wa wilaya hiyo na maeneo jirani kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na fursa hiyo adhimu ya kupimwa na kutibiwa bure.
Msando alisisitiza kuwa huduma hizo zitatolewa kwa wananchi wote bila ubaguzi, akiwahimiza wazazi na walezi kuhakikisha wanawaleta watoto wao pamoja na watu wenye changamoto mbalimbali za kiafya.
Afisa Uhusiano wa EACLC, Linda Mtui, kulia niMkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando.
Aliongeza kuwa huduma za afya kwa wanawake na watoto pia zitapewa kipaumbele, hatua inayolenga kugusa makundi nyeti ambayo mara nyingi hukosa huduma za uhakika kwa wakati.
Daktari bingwa kutoka China, Bao Zegtao kushoto niĀ Afisa Uhusiano wa EACLC, Linda Mtui.
Picha ya pamoja Mkuu Wa wilaya na Viongozi wa EACLC na madaktaria watakaotoa Huduma za afya jijini Dar es Salaam, kwa kuanzisha kambi maalum ya matibabu ya bure itakayodumu kwa siku mbili mfululizo, Machi 28 na 29, mwaka huu.




