Global Publishers
March 24, 2026
0 Comments
Diwani wa Kata ya Vighawe, Mpwapwa mkoani Dodoma, Emmanuel Ndule ameishukuru Global TV kwa jinsi ilivyosimamia suala la mwili wa Mtanzania Veronika Nyamwendo aliyefariki dunia akiwa Oman, unarudishwa nchini na kwenda kuzikwa kijijini kwao.
Amesema Global TV inasaidia wanyonge na kuiomba serikali iangalie namna ya kuishika mkono.
Pia amemshukuru Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene kwa kufanikisha mwili wa Veronika unarudishwa nchini na hatimaye kuzikwa.
Veronika alizikwa juzi kijijini kwao, Manghangu, Kata ya Vighawe, Mpwapwa mkoani Dodoma.