Wadau Washangazwa na Ukaribu wa Diamond na Lulu Diva

Global Publishers
March 24, 2026
0 Comments

Msanii nyota wa Bongo Fleva na Mkurugenzi Mtendaji wa WCB Wasafi, Diamond Platnumz, Machi 23, 2026 amezua gumzo mitandaoni baada ya kumpongeza Lulu Diva katika siku yake ya kuzaliwa kwa ujumbe ulioonekana kuwagusa wengi.

Kupitia comment aliyoiandika kwenye picha za Lulu Diva, Diamond alimtakia maisha marefu na yenye furaha, akisema: “Long Life Shem lake Mimi 🎂🤍🎉🎊”. Kauli hiyo imezua hisia mbalimbali miongoni mwa mashabiki na wadau wa burudani, huku wengi wakitafsiri ujumbe huo kama wa ukaribu na heshima ya kipekee kati ya mastaa hao wawili.

Sio Diamond pekee aliyeonyesha mapenzi kwa Lulu Diva katika siku yake hii maalum, bali pia wasanii na watu wa karibu wamejitokeza kumpongeza kupitia mitandao ya kijamii. Miongoni mwao ni Tessy Chocolate, Mac Voice, Sanchi pamoja na Lamatta, ambao wote wamemtakia heri na mafanikio mema katika maisha yake.

Lulu Diva ameendelea kupata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki na watu maarufu katika tasnia ya burudani, jambo linaloonyesha nafasi yake na mvuto wake katika muziki na filamu nchini Tanzania. Siku yake ya kuzaliwa imekuwa na mwitikio mkubwa mtandaoni, huku ujumbe mbalimbali zikiendelea kumiminika kutoka kwa watu tofauti.