Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imepitisha randama ya mpango na makadirio ya bajeti ya matumizi ya kawaida pamoja na mpango wa maendeleo kwa mwaka wa fedha 2026/2027 wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Mpango huo umepitishwa na kamati Machi 24, 2026 chini ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Husna Sekiboko, ambae amesema mpango huu unakwenda kuwa chachu ya kuandaa vijana wenye ujuzi.
Mhe. Sekiboko amesisitiza kuhakikisha mtiririko wa fedha utakaowezesha miradi yote ya maendeleo inatekelezwa na kukamilika kwa wakati.
” kwakweli tumeshuhudia miradi mingi mikubwa mizuri ambayo inajenga imani ya wananchi kwa Serikali na kuongeza tija katika maendeleo,” amesema Mhe Sekiboko
Pia ameiomba Wizara kushirikiana kwa Karibu na Wizara ya Fedha kuhakikisha fedha za miradi ya maendeleo kwa sekta ya elimu zinatolewa kwa wakati. Na kwa mtiririko unaowezesha utekelezaji wenye ufanisi.
Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda, amewashukuru wajumbe wa Kamati hiyo kwa kupokea na kupitisha randama ya bajeti ya wizara na kuahidi kuwa wizara itaendelea kuboresha mifumo na mazingira ya utoaji elimu ili kuhakikisha kila mtoto wa Kitanzania anapata elimu na ujuzi kwa usawa na ujumuishi.

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

