Mwanasiasa Mkongwe William Lukuvi Afariki Dodoma – Video

Global Publishers
March 25, 2026
0 Comments

Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, William Vangimembe Lukuvi enzi za uhai wake.

Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, William Vangimembe Lukuvi, amefariki dunia asubuhi ya Machi 25, 2026 akiwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Moses M. Kusiluka, Lukuvi alifariki kutokana na ugonjwa wa mshtuko wa moyo.

Marehemu Lukuvi aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, ikiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), pamoja na kuwa Mbunge wa Jimbo la Isimani kwa muda mrefu.

Alizaliwa Agosti 15, 1955, na alikuwa mmoja wa wabunge waliodumu kwa vipindi saba mfululizo tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1995 nchini Tanzania.

Kifo chake ni pigo kubwa kwa taifa, hasa katika nyanja za siasa na uongozi, ambapo alijijengea heshima kutokana na utumishi wake wa muda mrefu.