Waziri Mkuu Mwigulu Aeleza Masikitiko Yake Kufuatia Kifo cha Lukuvi – Video

Global Publishers
March 25, 2026
0 Comments

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwigulu Lameck Nchemba.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwigulu Lameck Nchemba, akiwa katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (PICC) kushiriki Mkutano wa 110 wa Wadau wa Elimu kwa Umma (WASHITIRI) leo Machi 25, 2026, ametoa salamu za pole kufuatia kifo cha aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Jimbo la Isimani, William Vangimembe Lukuvi, aliyefariki dunia majira ya saa moja asubuhi.

Taarifa ya kifo hicho ilitangazwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akieleza kuwa marehemu amefariki katika Hospitali ya Benjamin Mkapa alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa mshtuko wa moyo.

Rais Dkt. Samia ametuma salamu za pole kwa Spika wa Bunge, familia ya marehemu, wananchi wa Jimbo la Isimani pamoja na Watanzania wote kufuatia msiba huo mkubwa wa kitaifa.