Global Publishers
March 25, 2026
0 Comments
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewataka watayarishaji wa vipindi vya elimu kwa umma kuandaa maudhui yatakayowafikia na kuwagusa vijana kwa lugha wanayoielewa.
Dkt. Mwigulu amesema bila kutumia njia na lugha rafiki kwa vijana, taarifa muhimu zinaweza zisifikie walengwa au kushindwa kuwavutia.

Waziri Mkuu amesisitiza kuwa maudhui yanapaswa kuwa sahihi, ya kuvutia na yenye thamani ili vijana waweze kuyapokea na kufurahia kuyafuata.
Waziri Mkuu ametoa wito huo jijini Arusha leo Machi 25, 2026 wakati wa ufunguzi mkutano wa 110 wa Watayarishaji wa Vipindi vya Elimu kwa Umma (WASHITIRI) 2026 ambo umeandaliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), na kuwakutanisha wadau mbalimbali wa elimu kwa umma. Mdhamini Mkuu wa mkutano huo ni PSSSF pamoja na NSSF.

