Global Publishers
March 26, 2026
0 Comments
Mashindano ya kimataifa ya soka ya FIFA Series 2026 yanaanza rasmi leo Machi 26, 2026 jijini Kigali, huku Rais wa Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA), Fabrice Shema, akitangaza zawadi mbalimbali zitakazowania kuanzia kombe la ubingwa hadi tuzo ya mchezaji bora wa mashindano.
FIFA Series ni mpango mpya wa kimataifa ulioanzishwa na FIFA ili kutoa nafasi zaidi kwa timu za taifa kucheza mechi za kimataifa hasa zile ambazo hupata nafasi chache ya kukutana na timu kutoka mabara mengine.
Kuanzia leo, viwanja vya Amahoro na Kigali Pelรฉ vinakuwa kitovu cha soka duniani, huku mataifa nane yakishuka dimbani yakisaka ushindi na kujijengea heshima kimataifa.

Mashindano haya yanakusanya timu kutoka mabara tofauti, yakitoa nafasi kwa timu kujipima uwezo na kuongeza uzoefu wa kimataifa.
Timu shiriki zimepangwa katika makundi mawili
KUNDI A (Uwanja wa Amahoro)ย
๐ท๐ผ Rwanda (Wenyeji)
๐ฐ๐ช Kenya
๐ช๐ช Estonia
๐ฌ๐ฉ Grenada
KUNDI B (Uwanja wa Kigali Pelรฉ)ย
๐น๐ฟ Tanzania (Taifa Stars)
๐ฑ๐ฎ Liechtenstein
๐ฆ๐ผ Aruba
๐ฒ๐ด Macau
Mechi za leo (Machi 26):
๐น๐ฟ Tanzania ๐ ๐ฑ๐ฎ Liechtenstein (Uwanja wa Kigali Pelรฉ)
๐ฆ๐ผ Aruba ๐ ๐ฒ๐ด Macau (Uwanja wa Kigali Pelรฉ)
