Mapenzi Yamdatisha Kim Kardashian Aibuka Japan Kumshangilia Hamilton

Global Publishers
March 27, 2026
0 Comments

Staa wa reality TV Kim Kardashian akiwa na mpenzi wake, dereva wa Formula 1 Lewis Hamilton.

Staa wa reality TV Kim Kardashian anatarajiwa kumuunga mkono hadharani mpenzi wake, dereva wa Formula 1 Lewis Hamilton, kwa mara ya kwanza kwenye mashindano ya F1 nchini Japan.

Kim amewasili Japan akiwa na watoto wake wawili, Chicago na Psalm, kwa ajili ya kumshangilia Hamilton atakayeshiriki mbio hizo mwishoni mwa wiki hii.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu, safari hiyo ni ishara kwamba sasa wawili hao wako kwenye uhusiano wa wazi zaidi tofauti na hapo awali walipokuwa wakijisitiri.

Staa wa reality TV Kim Kardashian

Inadaiwa kuwa Kim aliwahi kuhudhuria mbio za Las Vegas Grand Prix mwaka jana lakini hakujionyesha wazi kumuunga mkono Hamilton kwa sababu uhusiano wao ulikuwa bado mpya.

Sasa mambo yamebadilika, ambapo wawili hao wameonekana wakitumia muda pamoja jijini Tokyo, ikiwemo kutoka kwa chakula cha jioni hali iliyowafanya mashabiki kuanza kuzungumzia zaidi mahusiano yao.

Mbali na mapenzi, Kim ameendelea kusisitiza juhudi zake za kusaidia jamii, hasa katika masuala ya haki za kisheria kwa wanawake. Ameeleza kuwa mapato ya baadhi ya miradi yake yatakwenda kusaidia wanawake wanaopigania haki zao mahakamani kupitia taasisi za msaada wa kisheria.

Kauli yake ilisisitiza kuwa kila mtu anapaswa kuwa na haki ya kupata wakili bila kujali uwezo wa kifedha.

Mashabiki Wasubiri Kuona Nini Kitafuata

Ujio wa Kim Japan umeongeza msisimko kuelekea mbio hizo, huku mashabiki wakisubiri kuona kama uwepo wake utampa motisha Hamilton kufanya vizuri zaidi uwanjani.

Inaripotiwa kuwa wawili hao wamekuwa marafiki kwa zaidi ya muongo mmoja kabla ya kuanzisha uhusiano wa kimapenzi, ambao sasa unaonekana kuwa imara zaidi.