Bakari Mahundu
March 28, 2026
0 Comments
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, katika matukio tofauti ya picha, alipoongoza Watanzania kuuaga mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Jimbo la Isimani, Marehemu William Lukuvi, katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Machi 28, 2026.

Katika hotuba yake, Rais Samia amewapa pole wanafamilia, ndugu na marafiki wa marehemu, huku akisisitiza mchango mkubwa aliouacha Lukuvi katika uongozi na utumishi wa umma. Amesema, “Hatutamsahau Mayele wetu,” akimlinganisha marehemu Lukuvi na mchezaji mahiri aliyewahi kuchezea Yanga, Fiston Mayele, kwa umahiri na mchango wake mkubwa.

Aidha, Rais Samia amegusia hali ya vita inayoendelea kati ya Iran, Marekani na Israel, akieleza kuwa kuna hatari ya kudorora kwa uchumi duniani kote, ikiwemo uchumi wa Tanzania, kutokana na athari za mgogoro huo.
Lukuvi alifariki dunia tarehe 25 Machi 2026 alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, mkoani Dodoma.