RAIS SAMIA: LUKUVI ALIJENGA MAHUSIANO MEMA YA KUDUMU NDANI YA JAMII

Na Janeth Raphael – MichuziTv 

Rais Samia amesema Taifa litamkumbuka William Lukuvi kama kiongozi aliyegusa maisha ya wengi kwa moyo wake wa upendo, hekima, na kujitolea kwa dhati katika utumishi wa umma.

“Hayati Lukuvi atabaki katika kumbukumbu zetu si tu kwa nafasi alizoshika, bali kwa namna alivyoweza kujenga mahusiano mema na ya kudumu ndani ya jamii”

Pia  Rais Samia amesema LUKUVI alikuwa kiongozi aliyesikiliza, aliyeshirikiana na makundi mbalimbali, na aliyethamini mchango wa kila mmoja katika kujenga taifa.

Katika kipindi hicho ambacho dunia inakumbwa na changamoto nyingi na mabadiliko yasiyotabirika, umuhimu wa kuwa na viongozi wenye uzoefu mpana na waliopitia ngazi mbalimbali za uongozi hauwezi kupuuzwa

 “Tulimuhitaji sana ndugu Lukuvi leo—zaidi hata kuliko jana—ili kuendelea kutoa mwongozo na busara katika nyakati hizi ngumu”

Aida Rais Samia amesema Maisha na utumishi wa  LUKUVI vinatufundisha somo muhimu sana: kwamba uongozi ni dhamana, si fursa ya kujinufaisha, n wajibu wa kuitumikia jamii kwa uaminifu, uwajibikaji, na moyo wa kujitolea bila kuchoka, Haya ndiyo maadili aliyoyaishi, na huu ndio urithi wake kwa taifa letu”

Hata hivyo Rais Samia amesema ni jukumu letu sasa kuuenzi na kuuendeleza urithi huo  Tuige mfano wake kwa kuimarisha mshikamano, kuheshimiana, na kufanya kazi kwa bidii kwa manufaa ya wote, kwa kufanya hivyo, tutakuwa tumemuenzi kwa vitendo, na kuhakikisha kuwa mchango wake unaendelea kuzaa matunda kwa vizazi vijavyo.