Mamilioni ya Wamarekani wameandamana katika miji zaidi ya 50 kote kote mwishoni mwa juma kupinga uvamizi wa pamoja wa Marekani na Israel dhidi ya Iran, wakati mzozo huo ukiingia mwezi wake wa pili.
Waandamanaji kutoka pwani hadi pwani walitoa wito wa kusitisha mara moja kwa vita dhidi ya Iran vilivyoanza tarehe 28 Februari.
Katika eneo la Manhattan, New York City, maelefu walikusanyika katika uwanja wa Union Square kulaani vita dhidi ya Iran.
Kaulimbiu kuu ya maandamano hayo ilikua “No Kings” (Hakuna Wafalme), ikimaanisha kuwa Wamarekani waliowengi sasa wanaamini kuwa Rais Donald Trump anatawala Marekani kwa mtindo wa kidikteta kama mfalme mwenye mamlaka kamili bila kuzingatia sheria na taasisi nyingine za nchi, hasa baada ya vita dhidi ya Iran bila idhini ya Bunge la Marekani (Congress).
Kaulimbiu nyingine zilijumuisha “Tishio Kubwa Zaidi Duniani Leo ni Donald Trump na Marekani na Trump Anasema Vita Zaidi, Sisi Tunasema Hapana Tena.
Waandamanaji walibeba mabango yaliyosomeka “Iacheni Iran, Hatutaki Vita Mashariki ya Kati na Fedha Zitumike Kukidhi Mahitaji ya Wananchi, Sio Vita Dhidi ya Iran.
Maya, mmoja wa waandamanaji katika uwanja huo, aliwaambia waandishi wa habari kwamba:
“Vita dhidi ya Iran havina haki. Ni vita vya kubadilisha utawala, na malengo ni ufisadi yaani aina ya ukoloni dhidi ya mataifa mengine na kuyatumia vibaya.”
Aliongeza kwa kusema: “Kwa ninavyoona, tunatumia takriban dola bilioni moja za Marekani kila siku katika vita wakati wananchi wanapokuwa na gharama ya maisha. Fedha hizo zinatakiwa kwa wananchi wa Marekani — kusaidia huduma za afya, malezi ya watoto, usafiri wa umma na chochote kile vita vya sasa.
Wazungumzaji katika mikutano hiyo walilaani dhidi ya Iran wakisema ukiukaji wa sheria za kimataifa na kuyataja kuwa chanzo cha kuleta Magharibi katika eneo la Asia.
Pia waliitaka Congress kuchukua hatua za haraka kusitisha operesheni hizo. Katika jiji la Los Angeles, maelfu walikusanyika nje ya City Hall wakipeperusha bendera za Iran na kupaza sauti kaulimbiu kama “Kudondosha Mabomu Iran ni Uhalifu.
Marekani na Israel zilianzisha kuanzisha makubwa dhidi ya Iran tarehe 28 Februari, jambo lililosababisha Iran kujibu kwa makombora na ndege zisizo na rubani zikilenga Israel na vituo vya kijeshi vya Marekani katika eneo la Asia Magharibi, linalojulikana pia kama Mashariki ya Kati.
Kushadidi vita kumezidisha wasiwasi wa kikanda na pia kuleta athari pana kimataifa, huku bei za petroli, dizeli na gesi zikiongezeka katika masoko ya dunia na zikitarajiwa kupanda zaidi katika siku zijazo.
Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limeonya kuwa vita dhidi ya Iran ambavyo vinaweza kuathiri wa kilimo na bei chakula, kwani wakulima wengi duniani kote petroli, dizeli na mbolea kutoka katika eneo la Mashariki ya Kati ambalo sasa limetumbukia katika vita kutokana na sera za kijinai za Marekani na utawala dhalimu wa Israel.