Bwege afariki dunia | Mwananchi

Dar es Salaam. Mwanasiasana aliyewahi kuwa Mbunge wa Kilwa Kusini, Selemani Said Bungara, maarufu Bwege, amefariki dunia leo Jumatatu, Machi 30, 3036 alipokuwa akipatiwa matibabu hospitalini.

Mkongwe huyo, ambaye Februari 18, 2026 alitangaza kujiondoa katika chama cha ACT-Wazalendo na kujiunga rasmi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amefikwa na umauti katika Hospitali ya EM iliyopo Mji Mwema, Kigamboni, jijini Dar es Salaam, alipokuwa akisubiri kupatiwa huduma ya matibabu.

Akizungumza na Mwananchi, leo Machi 30, 2026 ndugu yake aliyekuwa naye hospitalini hapo, Nasri Omari, amethibitisha kifo hicho akisema kuwa marehemu alifariki kabla ya kuanza kupatiwa matibabu.

“Amefariki wakati akisubiri kupata matibabu ya dialysis (huduma ya kusafisha damu), lakini kabla huduma hazijaanza, saa saba mchana hali yake ilibadilika ghafla na kufariki dunia,” amesema.

Amesema familia inaendelea na kikao cha ndani kupanga taratibu za mazishi, na taarifa rasmi zitatolewa kwa umma baada ya kukamilika kwa mazungumzo hayo.

Endelea kufuatilia Mwananchi