SELEMAN BUNGARA (BWEGE) MWENDO AMEUMALIZA

…..

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Kilwa Kusini kupitia Chama cha wananchi -CUF Selemani Bungara Maarufu Bwege amefariki dunia mchana wa leo wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya EM iliyopo Kigamboni Mkoani Dar es salaam.

Bwege alichaguliwa kuwa Mbunge wa Kilwa Kusini kwa mwaka 2015 – 2020 ambapo atakumbukwa alikuwa akichangia hoja mbali katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha baada ya kuhama chama cha CUF alikwenda katika Chama cha ACT Wazalendo ambapo hata hivyo hivi karibuni Alikihama chama Hicho na kwenda Chama cha Demokrasi na Maendeleo CHADEMA