…………..
NA Ester Maile Dodoma
Zaidi ya asilimia 80 ya Makaa ya Mawe yanayozalishwa nchini Tanzania yanauzwa nje ya nchi jambo linalopelekea raslimali hiyo kutochangia ipasavyo kwenye maendeleo ya viwanda, kuchelewesha mageuzi ya upatikanaji wa nishati, ukuaji wa uchumi na pato la taifa kama ambavyo yangetumika nchini
Hayo yamebainishwa hii leo Jijini Dodoma katika kikao cha wachimbaji, wafanyabiashara na wasafirishaji wa Makaa ya Mawe, na Tume ya madini kuwa sekta hiyo bado aichangii kikamilifu katika maendeleo ya taifa
Aidha, wadau hao wameitaka serikali kushugulikia changamoto 5 zinazowakabili, ikiwemo ongezeko la tozo bandarini, tozo za usafirishaji wa bidhaa hiyo pamoja na viwango vya bei ya mauzo ya malighafi hiyo
Naye Waziri wa Madini Antony Mavunde amesema, serikali itashugulikia changamoto zote zilizoainishwa na wadau hao ili kuhakikisha taifa linanufaika kikamilifu na uwepo wa makaa ya mawe

