MIXX BY YAS YAZINDUA WAKALA APP, UBUNIFU UNAOBADILI MFUMO WA UENDESHAJI WA MAWAKALA TANZANIA

Mafanikio haya yamejengwa juu ya uwazi, uaminifu, na huduma bora kwa wateja wetu, na ndiyo maana Mixx imethibitishwa na GSMA Mobile Money, ikithibitisha kuwa mifumo yetu inakidhi viwango vya juu vya kimataifa vya usalama, uwazi, na ulinzi wa taarifa za wateja.”

Akielezea kuhusu ubunifu huo mpya, Pesha alisema:

“Wakala App ni suluhisho ya kwanza sokoni inayowapa mawakala uwezo wa kusimamia biashara zao kwa ufanisi zaidi, kufuatilia utendaji kwa urahisi, na kuwa na udhibiti kamili wa shughuli zao za kila siku. Hii inaendana na dira yetu ya kujenga mfumo wa wakala wa kidijitali, wenye ufanisi na unaoweza kukua kwa kiwango cha juu.”

Sambamba na uzinduzi wa Wakala App, Mixx pia imeanzisha huduma ya mikopo kwa Mawakala wakuu inayowawezesha kupata mtaji wa kufanya kazi ili kukuza biashara zao na kuchangia maendeleo ya uchumi wa taifa.

Kupitia hatua hizi, Mixx inaendelea kuimarisha nafasi yake kama kiongozi wa ubunifu katika huduma za kifedha, kwa kuweka mkazo katika uwezeshaji wa mawakala, ufanisi wa huduma, na upatikanaji wa suluhisho za kisasa kwa Watanzania.

“Safari yetu ya mwaka huu ni ya ukuaji, ubunifu, na mafanikio ya pamoja. Tunaenda mbele tukiwa na zana bora zaidi, uwezo mkubwa zaidi, na maono makubwa zaidi ya mafanikio,” aliongeza Pesha.

Kwa kuwekeza katika teknolojia na uwezeshaji wa mawakala, Mixx inaendelea kujenga mfumo imara unaochochea ujumuishaji wa kifedha na maendeleo ya uchumi nchini Tanzania.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx by Yas, Angelica Pesha akizungumza na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa kwa mawakala wakubwa na washirika wa Mixx iliyofanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Hafla hiyo ilijumuisha pia uzinduzi wa huduma mpya ya Wakala App, jukwaa la kwanza la aina yake lililoundwa kubadilisha namna ambavyo mawakala wanaendesha biashara zao na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa zaidi ya wateja milioni 22 kote nchini, sambamba na kuanzishwa kwa huduma ya ‘Bustisha Wakala’ suluhisho la kifedha linalolenga kuwawezesha mawakala kupata mtaji wa kuendesha biashara zao. Hatua hii inaonesha dhamira endelevu ya Mixx ya kuendeleza ubunifu, kuwawezesha mawakala, na kukuza ujumuishaji wa kifedha nchini Tanzania.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Jabir Shekimweri (katikati), akikata utepe kuzindua rasmi wa duka la Yas katika kituo cha SGR jijini Dodoma jana, hii ikiwa ni sehemu ya juhudi za kampuni hiyo kupanua upatikanaji wa huduma za kidijitali na kifedha katika jiji la Dodoma linalokua kwa kasi. Pamoja nae ni Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja na Uendeshaji – Yas Tanzania, Bi. Mwangaza Matotola (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Yas – Kanda ya Kati, Said Idd (wa pili kulia), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano – TRC, Bw. Fredy Mwanjala (kushoto), pamoja na Mkuu wa Maduka ya Yas Tanzania, Bi. Sarah Sonelo.