Global Publishers
March 30, 2026
0 Comments
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema Serikali itachukua hatua madhubuti kushughulikia mapungufu yote yaliyobainishwa katika ripoti ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Akizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam leo Machi 30, 2026 baada ya kupokea ripoti hiyo, Rais Samia amesema amezipokea na kuzisikiliza kwa umakini taarifa zote zilizowasilishwa na taasisi mbalimbali za umma.
“Nimesikiliza kwa umakini ripoti na taarifa zote zilizowasilishwa. Napenda kutoa pongezi kwa CAG, Mkurugenzi wa TAKUKURU pamoja na PPRA kwa kazi kubwa wanazofanya. Taarifa zenu zinaonesha mafanikio lakini pia mapungufu katika baadhi ya maeneo yanayohitaji kuchukuliwa hatua,” amesema Rais Samia.

Ameongeza kuwa ripoti ya CAG imeonesha ongezeko la hati safi kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia wa 2023/2024, jambo alilosema linaashiria maendeleo makubwa katika usimamizi wa rasilimali za umma.
“Ni hatua nzuri inayoonesha namna tunavyoendelea kuboresha mikakati yetu ya matumizi ya rasilimali za umma. CAG ameainisha vizuri mapungufu pamoja na mapendekezo yake,” amesisitiza.
Rais Samia amehitimisha kwa kusema Serikali itachukua hatua kwa mujibu wa sheria na mapendekezo yaliyotolewa na CAG ili kuhakikisha mapungufu yote yanarekebishwa na malengo ya maendeleo yanafikiwa.
