*****
Mdhamini Mkuu wa mashindano ya Yanga Soccer School, Emwani Coffee Chini ya Mkurugenzi wake Leo Mendez amekabidhi Kombe la ubingwa wa mashindano ya Yanga Soccer School Kwa Timu ya TDS iliyopo chini ya kituo cha kuendeleza soka cha Shirikisho la Mpira Nchini TFF, baada ya kuifunga Timu ya FountainGate Academy katika mchezo uliochezwa katika viwanja vya KMC Jijini Dar es Salaam
Hafla ya kukabidhi kombe hilo iliyoongozwa na Makamu Wa Rais Ya Yanga Arafat Haji ilifanyika uwanja wa KMC mara baada ya mchezo wa fainali kati ya TDS waliobuka washindi kwa mikwaju ya penati dhidi ya Timu ya FontainGate Academy.
Fainali hiyo ni matokeo ya timu 16 zilizoanza kucheza katika hatua ya mtoano katika viwanja vya TFF kigamboni ambapo lengo la mashindano haya ya Yanga Soccer School ni Kutafuta vipaji vitakavyonolewa kwaajili ya kujiunga na mpango maalumu wa kuendeleza vipaji wa timu ya Yanga.
Katika Mashindano hayo Kampuni ya Emwani Coffee ilitoa udhamini wa vijana 10 ambao watachaguliwa na kujiunga katika Klabu Ya Yanga katika mpango wao maalumu ambao watakuwa na Udhamini wa asilimia zote kutoka kwa Emwani
Akizungumza katika Halfa Hiyo Mkurugenzi wa Emwani Coffee Leo Mendez Aliwapongeza mabingwa wa mashindano hayo ya Yanga Soccer School kuwa wanajivunia kuwa sehemu ya safari ya malengo ya vijana hawa wadogo ambao wanandoto za kulitumikia Taifa na kujikomboa kimaisha kupitia mpira ya miguu.
“Kipekee nimshukuru Rais wa Klabu ya Yanga Eng. Hersi Said Pamoja na kamati yake ya utendaji kwa kuipa nafasi Emwani Kuwa Mdhamini Mkuu wa Mashindano haya ambayo yana sura ya kimageuzi katika soka letu nchini na Sisi kama Emwani Tupo tayari kuendelea kuacha Alama ndani ya jamii na mioyo ya vijana wenye vipaji na uwezo wa kuleta mabadiliko chanya”
Katika Mashindano hayo Bingwa aliibuka na kiasi cha Shilingi Milion 3, mshindi wa pili Milion 1 na timu zilizoishia nusu fainali zilipata kiasi cha shilingi 500,000, pamoja na mfungaji bora, Kipa Bora na mchezaji bora wa mashindano wote walipatiwa zawadi ya pesa taslimu, Zawadi hizi zote ni udhamini wa Emwani Coffee.






