Makali bei za mafuta yaanza kung’ata Tanzania

Dar es Salaa. Athari za mapigano yanayoendelea katika nchi ya magharibi imeanza kung’ata nchini Tanzania kupitia ongezeko kubwa la bei za mafuta ambazo zitatumika Aprili mwaka huu, taarifa ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imeeleza.

Kushambuliwa kwa visima vya mafuta, maghala ya kuhifadhi mafuta na viwanda vya kusafisha mafuta pamoja na Iran kufunga lango la Hormuz linalopitisha takriban asilimia 20 ya mafuta yanayosafirishwa kwenda kwenye masoko mbalimbali duniani, imeathiri hali ya uzalishaji mafuta kwenye nchi za Mashariki ya Kati.

Kuathirika kwake kunaigusa moja kwa moja Tanzania ambayo inaagiza kwa kiasi kikubwa,jambo linalotajwa kuongeza gharama za usafirishaji kutokana na kukosekana kwa meli za kusafirisha mizigo na imeongeza gharama za bima za meli za mizigo kutokana na vita.

Kutokana na hali hiyo, sasa wanunuaji wa mafuta kwa bei ra rejareja yanayopitia Bandari ya Dar es Salaam watalazimika kuongeza Sh956 katika kila lita moja ya mafuta baada ya bei kufikia Sh3,820 kutoka Sh2864.

Kwa upande wa dizeli, lita moja sasa watanunua kwa Sh3,806 kutoka Sh2,858 ikiwa ni ongezeko la Sh948.

Kwa upande wa mafuta ya taa, sasa yatanunuliwa kwa Sh3,684 kutoka Sh2,932 iliyokuwa ikitumika Machi mwaka huu ikiwa ni ongezeko la Sh752.

Kwa upande wa watumiaji wa mafuta ya petroli yanayopitia katika bandari ya Tanga, nao wataugulia maumivu kama wenzao kwani sasa lita moja itauzwa kwa Sh3,881 kutoka Sh2,925 ikiwa ni ongezeko la Sh956 kwa kila litta.

Wanaotumia mafuta ya dizeli yanayopita katika bandari hiyo sasa watanunua lita moja kwa Sh3,867 Aprili mwaka huu kuttoka Sh2,919 iliyotumika Machi mwaka huu, ikiwa ni ongezekoo la Sh948 kwa lita.

Wale wa mafuta ya taa nao watalazimika kuongeza Sh752 kwa kila lita baada ya mafuta kufikia Sh3,745 kutoka Sh2,993.

Wakazi wa Mtwara ndiyo wenye makali zaidi kuliko wengine wote baada ya viwangoo vya bei ya mafuta yanayopita katika bandari hiyo kuwa juu ukilinganisha na bandari nyingine.

Hiyo inafanya sasa wanunuzi wa mafuta ya rejareja kutumia Sh3,912 kupata lita moja ya petroli, ikiwa ni ongezeko la Sh956 kutoka bei iliyokuwapo Machi mwaka huu.

Mafuta ya dizeli nayo yalifikia Sh3,898 kutoka Sh2,951 iliyokuwapo Machi mwaka huu, ikiwa ni ongezeko la Sh947 huku mafuta ya taa yakifikia Sh3,777 kwa lita kutoka Sh3,025 iliyokuwapo Machi mwaka huu ikiwa ni ongezeko la Sh752.

Kwa mujibu wa Ewura, ongezeko hilo la bei za mafuta ni janga la kidunia na Tanzania kama sehemu hiyo inachukua hatua mbalimbali kuhakikisha usalama wa upatikanaji wa mafuta nchini na katika bei himilivu ili kupunguza madhara ya kiuchumi na kijamii.

Kutokana na hali hiyo, wananchi wanashauriwa kutumia mafuta kwa uangalifu na ufanisi mkubwa.

Ongezeko la bei ya mafuta halipo Tanzania pekee, bali hata katika soko la dunia ambapo bei kikomo kwa Aprili 2026, zimeongezeka kwa asilimia 69.98 kwa mafuta ya petroli, asilimia 114.46 kwa mafuta ya dizeli na asilimia 120.81 kwa mafuta ya taa.

Kwa upande wa gharama za uagizaji kwa Aprili 2026, gharama za kuagiza mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam zimeongezeka kwa wastani wa asilimia 5.3 kwa mafuta ya petroli na asilimia 10.8 kwa mafuta ya dizeli na hakuna mabadiliko ya gharama kwa mafuta ya taa.

Katika Bandari ya Tanga gharama zimeongezeka kwa asilimia 6.9 kwa mafuta ya petroli na hakuna

“Hata hivyo, kwa bei za Aprili 2026, wastani wa gharama za kubadilisha fedha za kigeni zimepungua kwa asilimia 0.45,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.