Global Publishers
April 1, 2026
0 Comments
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza ongezeko kubwa la bei za mafuta nchini, ambapo kwa Jiji la Dar es Salaam, bei ya petroli imepanda kwa Sh956 kwa lita—kutoka Sh2,864 mwezi Machi hadi kufikia Sh3,820 mwezi Aprili 2026.
Kwa mujibu wa EWURA, bei hizo mpya zimeanza kutumika rasmi kuanzia leo Jumatano, Aprili 1, 2026.
Ongezeko hilo linatajwa kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na hali ya sintofahamu katika soko la kimataifa la mafuta, hususan kutokana na mvutano wa kijeshi unaoendelea Mashariki ya Kati unaohusisha Marekani, Israel na Iran.
Kwa kawaida, bei za mafuta nchini Tanzania hutegemea zaidi gharama za uagizaji kutoka soko la dunia pamoja na mabadiliko ya thamani ya fedha za kigeni, hali inayofanya bei kupanda au kushuka kulingana na mwenendo wa kimataifa .
Kupanda huku kwa bei kunatarajiwa kuongeza gharama za maisha kwa wananchi, kwani mafuta ni mhimili muhimu katika usafirishaji na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali.
