


Chikola ajishtukia mapema Yanga | Mwanaspoti
YANGA inaendelea kujifua kwenye kambi yao iliyopo Avic Town, Kigamboni chini ya kocha Romain Folz, lakini kuna winga mmoja mpya aliyetua klabuni hapo hivi karibuni amejishtukia baada ya kukiangalia kikosi hicho na fasta akaamua kujiongeza mwenyewe ili mambo yawe mepesi. Nyota huyo ni kiungo mshambuliaji aliyetua Jangwani kutoka Tabora United, Offen Chikola amesema kwa namna…

DKT. NCHIMBI AWANADI WAGOMBEA UBUNGE, MADIWANI WA SIMIYU KWA WANANCHI
MGOMBEA mwenza wa kiti cha urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),Balozi Dkt.Emmanuel John Nchimbi amepokelewa kwa shangwe na wananchi alipokuwa akiwasili katika uwanja wa CCM,wilaya ya Bariadi Vijijini mkoani Simiyu kuendelea na mkutano wa Kampeni, leo Jumatatu Septemba 1,2025. Dk.Nchimbi aliyekuwa Mkoa wa Mara na sasa ameingia Mkoa wa Simiyu kuendelea na kampeni,akianzia…

WIZARA YA ARDHI YAPATA TUZO KUTOA WASHIRIKI WENGI MKUTANO WA TRAMPA 2025
……. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imepata tuzo kwa kuwa miongoni mwa Wizara zilizotoa washiriki wengi kwenye Mkutano Mkuu wa Chama cha Menejiment ya Kumbukumbu na Nyaraka (TRAMPA). Wizara ya Ardhi ilitoa watumishi 56 kushiriki mkutano huo wa kitaaluma uliofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Tuzo hiyo ilikabidhiwa…

WAMILIKI WA SILAHA WATAKIWA KUSALIMISHA SILAHA ZAO
………. JESHI la Polisi limewataka watu wote wanaomiliki silaha haramu kinyume na sheria kuzisalimisha kwa hiyari kunzia Sepetemba 01, hadi Oktoba 31, mwaka huu ambao ndiyo muda wa msamaha ulitolewa na Serikali. Msemaji Mkuu wa Jeshi hilo David Misime, alisema hayo leo jijini Dodoma, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu msamaha wa kutoshitakiwa kwa…

NIRC YAWEKA KAMBI KUCHIMBA VISIMA 52 VYA UMWAGILIAJI TABORA John Bukuku Last updated: 2025/09/01 at 2:38 PM John Bukuku 4 hours ago Share
…………. NIRC:Nzega Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imeanza uchimbaji wa visima 52 katika halmashauri nane za Mkoa wa Tabora. Ili kuwezesha wakulima wa maeneo hayo kuacha kulima kilimo cha mazoea ya kugemea msimu wa mvua na kujikita katika kilimo cha kisasa cha umwagiliaji. Katika kijiji cha Miguwa, visima vitakavyochimbwa vitamwagilia zaidi ya ekari…

Kampeni zaendelea, vyama vitatu vikisuasua
Dar/Mikoani. Wakati Chama cha Demokrasia Makini kikizindua kampeni zake za uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kesho Jumanne, vyama vinne vimepishana na ratiba ya uzinduzi wa kampeni zao iliyotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), huku Chama cha Mapinduzi (CCM) kikiendelea kujinadi kwa wananchi. Wakati kampeni zikiingia siku ya tano leo tangu zianze Agosti…

Ahadi hewa mwendokasi Mbagala zakera wakazi Dar
Dar es Salaam. Baada ya huduma ya mabasi yaendayo haraka (mwendokasi) katika barabara ya Mbagala kukwama kuanza leo kama ilivyoahidiwa awali na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), wachumi na wadau mbalimbali wamejitokeza kutoa malalamiko pamoja na ushauri wa nini kifanyike ili huduma hiyo ianze kutekelezwa. Akieleza sababu ya kushindwa kutimiza ahadi hiyo, alipozungumza na…

Sababu wanawake kuwa vinara wa mikopo
Dar es Salaam. Kwa mara ya kwanza nchini, wanawake wanamiliki akaunti za mikopo ya kidijitali nyingi zaidi kuliko wanaume, jambo linalowafanya kuwa wakopaji wakuu katika sekta ya teknolojia ya fedha inayokua kwa kasi. Takwimu mpya kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Ofisi za Taarifa za Wakopaji (Credit Reference Bureaus) zinaonesha idadi ya akaunti za…

Hizi hapa ahadi za Dk Nchimbi kwa wananchi Simiyu
Busega. Wakati mgombea mwenza wa urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Emmanuel Nchimbi akiwaahidi wana Busega, mkoani Simiyu miradi mbalimbali, wananchi nao wamekitaka chama hicho kuzitekeleza kwa vitendo. Wamesema kuahidi ni jambo moja na kuzitekeleza ni suala jingine, hivyo mgombea Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wanapaswa kuhakikisha ahadi hizo zinatekelezwa ndani ya miaka…