
Polisi waendelea kumsaka mganga anayedaiwa chanzo cha kifo cha mwanafunzi
Arusha. Zikiwa zimepita siku 17 tangu kufariki dunia kwa mwanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Qash iliyopo wilayani Babati, mkoani Manyara, Yohana Konki (17), Jeshi la Polisi mkoani Manyara limesema linaendelea kumsaka mganga wa kienyeji anayedaiwa kutoa ramli chonganishi iliyosababisha mauaji hayo. Yohana, alifariki dunia baada ya kupigwa na wanafunzi wenzake kwa…