‘Simu, TV sio malezi, unyanyasaji kwa wanawake bado changamoto’
Ruangwa. Wazazi na walezi wametakiwa kuwalea watoto katika maadili yanayoendana na dini zao badala ya kuwaachia simu za mkononi na televisheni kuamua malezi yao. Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Zainab Telack, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika katika Kijiji cha Mbekenyera, wilayani Ruangwa leo Jumapili, Machi 8, 2026….