Vifo vya wajawazito, watoto vyapungua Maswa
Maswa. Vifo vya wajawazito katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa vimepungua kwa kiasi kikubwa kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo, kutoka vifo vinane hadi viwili, hatua inayotajwa kuwa mafanikio ya uwekezaji katika sekta ya afya. Kupungua huko kunatajwa kuchangiwa na kuimarika kwa huduma za afya, ikiwemo upatikanaji wa huduma za upasuaji wa dharura, ujenzi wa…