Kituo cha taarifa mwarobaini kero za wananchi Mbarali
Mbarali. Wananchi wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wameeleza matumaini yao baada ya Serikali kufungua Kituo cha Taarifa (Call centre), wakisema kitawasaidia kupunguza gharama za kusafiri umbali mrefu kuwasilisha kero na kupata ufumbuzi. Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti leo Jumamosi, Machi 7, 2026, katika Kata ya Igurusi, wamesema ujio wa mfumo huo utasaidia kuokoa muda…