Waliopata maafa ya mvua Kahama kupatiwa misaada ya kibinadamu
Shinyanga. Kufuatia nyumba zaidi ya 200 ikiwemo zahanati ya kijiji cha Mwanase Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga kubomolewa na mvua usiku wa kuamkia Desemba 13,2025, Serikali mkoani humo imeielekeza Halmashauri ya Msalala kufikisha mara moja misaada ya kibinadamu katika eneo hilo. Mvua hizo zilisababisha kuezuliwa kwa mapaa katika nyumba 127 huku nyumba 80 zikibomoka kabisa…