


Mahakama Kenya yazuia ujenzi wa kanisa Ikulu
Dar es Salaam. Mahakama Kuu nchini Kenya imeamuru kusitishwa kwa muda ujenzi wa kanisa la kudumu au jengo lolote la kidini katika majengo ya Ikulu, nchini humo. Agizo hilo la muda pia linazuia ujenzi kama huo katika Ikulu za Rais zilizoko maeneo mbalimbali nchini au hata jengo lolote lenye mafungamano na dini. Kwa mujibu wa…

WATALAAMU WA UFUATILIAJI NA TATHMINI WIZARA YA MALIASILI WAHIMIZWA KUWA KIDIGITALI
…………….. Na Sixmund Begashe, Dodoma Wataalam wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Maliasili na Utalii wametakiwa kuzingatia matumizi ya mifumo ya kidijitali katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuongeza ufanisi katika uchakataji, uhifadhi na upatikanaji wa taarifa kwa wakati. Wito huo umetolewa jijini Dodoma na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara…

BHOJANI AMWOMBEA KURA RAIS DK.SAMIA KISUTU
MGOMBEA Udiwani wa Kata ya Kisutu, Tousif Bhojani, amewataka wananchi wa kata hiyo kumpa kura za kishindo mgombea urais kwa kitekiti ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika uchaguzi mkuu wa Okotoba 29 mwaka huu. Ameyasema hayo Dar es Salaam, leo baada ya kurejesha fomu ya uteuzi wa udiwani katika Ofisi…

Yaliyojiri shauri la Mpina kugombea urais
Dar es Salaam. Shauri la utata wa uteuzi wa mgombea urais wa chama cha ACT-Wazalendo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 limetajwa mahakamani kwa mara ya kwanza, huku Mahakama ikisema haitasita kusimamia haki itakaporidhika kuhusu uwepo wa ukiukwaji wa taratibu. Shauri hilo limefunguliwa jana, Agosti 27, 2025, Mahakama Kuu, Masjala Kuu Dodoma, na Bodi ya…

Kicheko na maumivu wagombea ubunge, udiwani wakipenya INEC
Mikoani. Ni kicheko na maumivu kwa wagombea wa nafasi ya ubunge na udiwani baada ya baadhi kuteuliwa na wengine kukosa sifa ya kuteuliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuanza safari ya kusaka kura kuwaongoza wananchi ngazi ya kata na jimbo. Wagombea wa ubunge Jimbo la Moshi Vijijini kutoka chama Makini na Jimbo…

Wagombea udiwani 16 CCM kupigiwa kura za ndiyo au hapana uchaguzi mkuu Kigoma
Kigoma. Wakati kampeni zikianza kote nchini katika nafasi za ubunge, udiwani na urais, Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Kigoma wagombea udiwani katika kata 16 wanatarajiwa kupigiwa kura za ndiyo au hapana baada ya vyama vya upinzani kutosimamisha wagombea katika kata hizo. Mkoa wa Kigoma una jumla ya kata 139 ambapo kuelekea uchaguzi mkuu mwezi oktoba…

Wataja mbinu kuboresha elimu watu ya wazima
Dar es Salaam. Wataalamu mbalimbali wa elimu nchini wametoa mapendekezo manne ya kuboresha Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Tanzania (TEWW). Miongoni mwa mapendekezo hayo ni pamoja na Serikali kuandaa waraka utakaowasaidia wanafunzi wanaotoka nje ya mfumo rasmi wa elimu, kurudi kwenye masomo kupitia taasisi hiyo kwa lazima. Pia, wamependekeza Serikali kuandaa waraka wa elimu…

INEC YAONDOA FOMU ZA UTEUZI ZA WAGOMBEA KITI CHA RAIS NA MAKAMU WA RAIS KATIKA UBAO WA MATANGAZO
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg. Ramadhani Kailima (kulia) ameongoza watumishi wa Tume kuondoa fomu za uteuzi wa wagombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ubao wa matangazo wa Tume ikiwa zimepita saa 24 za kubandikwa fomu hizo ikiwa ni utekelezaji wa masharti ya sheria….

CAG AFANYA ZIARA ENEO LA HIFADHI YA NGORONGORO
Na Hamis Dambaya, Ngorongoro. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Charles Kichere ametoa wito kwa watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia sheria, taratibu, kanuni na kushirikiana ili kulinda matumizi sahihi ya rasilimali za umma. Akizungumza na menejimenti ya Ngorongoro, Kichere amesema njia pekee ya taasisi kufanya…