Kutolipwa michango EAC, mawaziri wapewa zigo kulitatua
Arusha. Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), limepewa jukumu la kupitia upya mfumo wa michango ya kifedha ya nchi wanachama na kupendekeza upya makadirio inayopaswa kulipwa itakayolingana na uwezo halisi wa kiuchumi wa kila nchi. Hatua hiyo imekuja kufuatia kuchelewa mara kwa mara kwa baadhi ya nchi kuwasilisha michango yao ya uanachama,…