Serikali kukamilisha maandalizi mkakati kukabiliana na wanyama wakali
Arusha. Serikali imesema inaendelea kukamilisha maandalizi ya Mkakati wa Kitaifa wa Kukabiliana na Wanyamapori Wakali na Waharibifu (2025/26–2034/35) pamoja na kufanya tafiti za kimkakati ili kubuni mbinu mpya za kukabiliana na wanyamapori hao, hususan tembo. Aidha, imeielekeza Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (Tawiri) kuendelea kuwafunga mikanda ya mawasiliano tembo viongozi ili kubaini mienendo yao…