Mahakama Kuu Yakataa Pingamizi, Kesi ya Uchaguzi Kigoma Mjini Kuendelea
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Kigoma, imeamua kuendelea na Shauri la Uchaguzi Namba 28949 la Mwaka 2025, baada ya kutupilia mbali pingamizi la awali lililowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na Clayton Revocatus Chipando, maarufu kama Baba Levo. Uamuzi huo umetolewa leo Desemba 16, 2025, na Mahakama ikiongozwa na Mheshimiwa Jaji Projestus…