
Bado Watatu – 6 | Mwanaspoti
“NIKAITAZAMA namba yake na kuiandika kwenye notibuku yangu kisha nikaingia upande wa meseji zilizotoka ambazo aliziandika marehemu mwenyewe.Huko nilikuta meseji kadhaa lakini nilizozitilia maanani zilikuwa meseji mbili ambazo aliziandika katika tarehe ya jana yake.Moja iliuliza.“Nyumbani wapi?”Ya pili ikauliza.Utakuja saa ngapi?”Nikahisi kwamba meseji hizo zilikuwa majibu ya zile meseji zilizotumwa ambazo moja zilisema; “Itabidi nije nyumbani…