
Maganda ya miwa yalivyogeuka fursa ya mkaa mbadala Zanzibar
Unguja. Wakati Tanzania ikiendelea kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa nishati safi ya kupikia, kundi la vijana wa Pangawe, Unguja, limebuni teknolojia ya kutumia maganda ya miwa kuzalisha mkaa mbadala. Ubunifu huo unatajwa kuwa suluhisho muhimu kwa kulinda mazingira, kuboresha afya za watumiaji na kutoa ajira kwa vijana. …