
COPRA YATOA UFAFANUZI WA MWENENDO WA SOKO LA MBAAZI DUNIANI
MAMLAKA ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) imetoa ufafanuzi kuhusu mwenendo wa soko la mbaazi duniani, ikieleza mafanikio na changamoto zinazolikumba zao hilo muhimu kwa wakulima wa Tanzania. Mkurugenzi Mkuu wa COPRA, Bi. Irene Mlola, amesema kuwa licha ya kushuka kwa bei ya mbaazi katika soko la kimataifa, wakulima wa Tanzania bado wananufaika…