Mbuni atwaa taji la ndege wa mwaka 2026 Tanzania
Arusha. Mbuni amechaguliwa kuwa ndege wa Mwaka 2026, baada ya kuibuka mshindi katika kura za kitaifa zilizoshirikisha wapenzi wa ndege nchini na kimataifa, akimrithi ‘kwezi maridadi’ (Superb Starling), aliyeshikilia taji hilo kwa mwaka 2025. Ndege huyo mkubwa zaidi duniani, ametwaa heshima hiyo baada ya kuwashinda washindani wake wanne maarufu wa uwanda wa nyasi katika kampeni…