


Rais Samia amteua Makalla RC Arusha
Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan leo Jumamosi, Agosti 23, 2025 amemteua Amos Makalla kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha (RC) kuchukua nafasi ya Kenani Kihongosi. Awali, Makalla alikuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM) nafasi ambayo Halmashauri Kuu ya CCM, imemteua Kihongosi kuishika. Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano…

Mastaa Stars waondoka CHAN kibosi
TANZANIA ikiwa mwenyeji wa CHAN 2024 ikishirikiana na Kenya na Uganda, imeaga mashindano baada ya kuondolewa na Morocco katika hatua ya robo finali lakini mastaa wa timu hiyo wamendoka na mkwanja wa maana usipime. Stars ya awamu hii ilikuwa na mvuto wa aina yake kuanzia namna inavyocheza na zaidi ikaweka rekodi ya kucheza robo fainali…

Hii hapa orodha kamili waliopenya ubunge, uwakilishi CCM
Katika kikao chake kilichofanyika leo Jumamosi, Agosti 23, 2025, NEC imepitisha majina ya wagombea watakaosimama majimboni kote nchini, sambamba na wawakilishi wa viti maalum kwa makundi maalum ya kijamii.

Makalla awekwa kando CCM, Kihongosi amrithi
Dar es Salaam. Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imemteua Mkuu wa Mkoa wa Arusha (RC), Kenan Kihongosi kuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafuzo wa chama hicho. Kihongosi anachukua nafasi ya Amos Makalla ambaye ameachwa. Uteuzi huo umefanyika leo Jumamosi, Agosti 23, 2025 katika kikao cha Halmashauri Kuu kilichoongozwa na Mwenyekiti wa chama…

Watano kati ya 19 waliokuwa wabunge Chadema wateuliwa CCM
Dar es Salaam. Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imewateua miongoni mwa waliokuwa wabunge 19 wa Chadema kuwania ubunge. Wabunge hao baada ya Bunge la 12 kuvunjwa walihamia CCM na kujitosa kwenye majimbo. Walioteuliwa na majimbo yao ni Esther Matiko (Tarime Mjini), Ester Bulaya (Bunda Mjini), Hawa Mwaifunga (Tabora Mjini), Kunti Majala (Chemba) na…

Dk Asha Rose – Migiro katibu mkuu mpya CCM
Dar es Salaam. Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imemteua Dk Asha Rose-Migiro kuwa katibu mkuu mpya wa chama hicho, kuchukua nafasi ya Dk Emmanuel Nchimbi ambaye ni mgombea mwenza wa urais wa CCM. Uteuzi wa Dk Migiro aliyewahi kuwa naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), umetangazwa na Katibu wa Itikadi, Uenezi…

Askofu Mapunda asisitiza haki kuelekea uchaguzi mkuu
Mbeya. Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Singida, Edward Mapunda amewatahadharisha Watanzania kutorubuniwa kwa rushwa na kuomba haki itendeke kwenye uchaguzi mkuu Oktoba 29 mwaka huu wa kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani na kusisitiza atakayeshinda ashinde kwa haki. Hatua hiyo imetajwa ni kuhepusha migogoro sambamba na kusisitiza watakao shindwa wakubali matokeo ili kulinda amani ya…

WANANCHI MBAGALA WANASWA KWA WIZI WA UMEME TANESCO
…………….. Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Temeke limewakamata baadhi ya wateja wake katika eneo la Mbagala Zakhiem kwa tuhuma za wizi wa nishati ya umeme pamoja na uharibifu wa miundombinu, ikiwemo kuharibu mifumo ya LUKU jambo ambalo ni kinyume cha sheria na taratibu za matumizi ya umeme. Akizungumza Agosti 22, 2025 jijini Dar…

Masoud: Zanzibar inahitaji mabadiliko | Mwananchi
Dar es Salaam. Mtiania wa urais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kupitia chama cha ACT- Wazalendo, Othman Masoud Othman amesema Zanzibar inahitaji mageuzi ya kiuchumi, kijamii na kisiasa, ambayo yanamsukuma kuwania nafasi hiyo. Othman ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, amesema hayo leo Agosti 23, 2025 alipozungumza na wahariri wa vyombo…