REA NYUMBA KWA NYUMBA VITONGOJINI MTWARA
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unaendelea na Kampeni ya kuhamasisha wananchi kuunganishiwa umeme sambamba na kuutumia kujiletea maendeleo. Kampeni hiyo inafanyika kupitia njia mbalimbali ikiwemo Mikutano ya hadhara na wananchi vitongojini pamoja na kuwatembelea wananchi nyumba kwa nyumba, taasisi kwa taasisi kuwahamasisha, kuwaelimisha hatua na taratibu za kuvuta umeme na elimu ya ulinzi na utunzaji…