Wakuu wa vyombo vya habari watoa tamko kulinda amani, Manyerere alikosoa
Dar es Salaam. Wakuu wa vyombo vya habari na wahariri waandamizi nchini wamepitisha azimio la amani wakisisitiza kulinda amani, maadili ya kitaaluma na mshikamano wa kitaifa kuelekea uchaguzi mkuu. Azimio hilo lililotiwa saini na viongozi wa vyombo vya habari leo Jumamosi Oktoba 25, 2025, limeainisha mambo 12 ya msingi katika kuhakikisha Taifa linaendelea kudumisha amani…