Ulega aagiza vibarua kupatiwa vyeti baada ya kumaliza kazi
Iringa. Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amewaagiza wahandisi, makandarasi na kampuni zinazotekeleza miradi ya Serikali, kuhakikisha kila fundi au kibarua anayeshiriki katika miradi hiyo anapewa cheti maalumu baada ya kukamilika kwa mradi, kinachoonesha amefanya kazi husika. Agizo hilo amelitoa leo Alhamisi Februari 26, 2026, wakati wa ziara yake katika mradi wa ujenzi wa jengo la…