NIKWAMBIE MAMA: Mzalendo ni gaidi wa kaburu
Siku moja Mwalimu Nyerere alisema kuwa aliona wakubwa wakienda kufanya azimio Zanzibar. Alipowaona wakirudi kimya kimya na sera za uchumi zikibadilika kufuata matakwa ya WB na IMF, akawa na uhakika kuwa ndoto zake za Azimio la Arusha zilikuwa zimefikia ukingoni. Mwenyewe alijua fika kuwa Azimio la Arusha lilikuwa ni chukizo kubwa kwa wakoloni na wanyonyaji….