FCC Kuendelea na Michakato ya Sheria Kuimarisha Ushindani wa Soko
Tume ya Ushindani (FCC) imesema itaendelea na mchakato wa marekebisho ya sheria zake kwa lengo la kuimarisha ulinzi wa walaji, kudhibiti bidhaa bandia na kuhakikisha kunakuwepo ushindani wa haki unaochochea ukuaji wa uchumi na ajira nchini. Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Khadija Ngasongwa, wakati akifungua semina ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari…