Wataalamu wataja sababu ongezeko la mafua, Uviko-19
Dar es Salaam. Wakati Wizara ya Afya ikitoa tahadhari kwa wananchi kufuatia ongezeko la wagonjwa wa mafua makali na Uviko-19 nchini, wataalamu wa afya wameeleza sababu za kuongezeka kwa maambukizi hayo katika kipindi hiki. Aidha, wataalamu hao wametaja makundi yaliyo hatarini zaidi na kusisitiza umuhimu wa kupata matibabu stahiki mapema, badala ya kujitibu bila ushauri…