Mauaji ya msemaji M23 yadhoofisha mazungumzo ya Qatar kusitisha mapigano DRC
Dar es Salaam. Kuuawa kwa msemaji wa kundi la waasi la M23, Willy Ngoma, kunatajwa kuwa mwanzo wa kutetereka kwa mazungumzo ya kusitisha mapigano yanayoongozwa na Qatar, ikiwa ni jitihada za kusaka amani ya kudumu Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC). Ngoma ameuawa katika shambulizi la ndege zisizo na rubani mashariki mwa DRC…