ONGEA NA ANTI BETTI: Mke wangu amenifumania, amekaa kimya
Anti ninashindwa niseme au nifanye nini kwani maana mke wangu anataka kuniua kwa kihoro. Nilikuwa na uhusiano na rafiki yake (nimeacha na sitorudia tena usiniseme vibaya), amejua maana alikuta ujumbe mfupi wa mahaba akaniuliza nikakataa. Nadhani alikuwa anatufuatilia kwani alitukuta uso kwa macho tukiwa hotelini nje ya mji tunaogelea kwenye jakuzi. Siyo jakuzi la jumuia…