
Jeshi la Polisi lilivyoyazima maadhimisho ya Chadema
Dar/Mikoani. Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yaliyoandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hayakufanyika, baada ya viongozi wake wa ngazi ya kanda kujikuta mikononi mwa polisi, huku wengine wakizuiliwa kufika eneo la tukio. Hata hivyo, alipotafutwa Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime, kuzungumzia matukio hayo, simu yake iliita bila kupokelewa, na hata alipotumiwa…