Lissu aomba kuirahisishia kazi Jamhuri ushahidi wa kesi yake
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, ameiomba Jamhuri isihangaike kuwaita mashahidi kuthibitisha baadhi ya vielelezo vya ushahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili, akisema kuwa hana shida navyo. Lissu amewasilisha ombi hilo mahakamani baada ya kusomewa shtaka la uhaini linalomkabili na kujibu, kisha akasomewa maelezo ya awali ya kesi…