Bado Watatu – 35 | Mwanaspoti
Raisa alifanya kazi ya ziada kunibembeleza ninyamaze na akanipa moyo kwamba yaliyonitokea ni mitihani tu na kwamba Mungu ataniepushia balaa. Muda wa kulala ulipowadia, Raisa alinikaribisha chumbani mwake. Raisa hakuwa na mume, lakini nilipoingia chumbani mwake niliona suruali ya kiume aina ya jeans imetundikwa kwenye mlango. “Mbona kuna suruali ya kiume humu ndani?” nikamuuliza. “Nina…