Watatu kortini wakidaiwa kusafirisha kilo moja ya cocaine
Dar es Salaam. Wafanyabiashara watatu, wakazi wa Manzese, jijini Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakidaiwa kusafirisha kilo moja ya dawa za kulevya aina ya cocaine. Washtakiwa hao ni Salum Kilindo (46), Salum Hassan (33) na Sofia Ngawaya (34). Leo Ijumaa, Septemba 19, 2025, washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo na kusomewa…