Bado Watatu – 29 | Mwanaspoti
BAADA ya kunipakia kwenye pikipiki nilimwambia: “Mdogo wangu, usipende kujitia katika mambo yasiyokuhusu. Hata kama hiyo namba ya gari umeiona, usiiseme — unaweza kuja kupata matatizo.”“Kaka yangu amenionya sana. Achilia mbali namba, hata kueleza kuwa nimeliona hilo gari nimekoma.”“Wakati mwingine polisi wanaweza kukurubuni ili uwatajie.”“Hao polisi watanijuaje?”“Huyo msichana aliyekupigia simu anaonekana ana kidomodomo sana.”“Nitamkana mchana…